Nasaha kwa mwanamke anayedhulumiwa na mume wake


Swali: Mwanamke huyu anasema kuwa ameolewa na mwanaume ambaye anamdhulumu kwa kutumia mkono wake na ulimi wake. Ni ipi nasaha yako na afanye nini?

Jibu: Nasaha yangu awe na subira huenda Allaah akamwongoza na akamuondoshea madhara kwake. Jambo la pili ikiwa hawezi kuwa na subira aombe kutengana mahakamani kwa Qaadhiy. Qaadhiy ataangalia hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13817
  • Imechapishwa: 20/09/2020