Nasaha kwa msichana asiyetaka kuolewa na mchumba anayemshinda umri

Swali: Mimi ni msichana amekuja kijana kunichumbia ambaye ni mdogo kwangu kwa miaka mitatu. Katika mila na desturi za watu katika nchi yetu ni kwamba mwanamke hawi mkubwa kiumri kumshinda mumewe. Ninachelea desturi hizi za watu kuathiri katika ndoa yetu. Unaninasihi nini endapo mwanaume huyo atakuwa ni mtu amenyooka katika dini? 58

Jibu: Nakunasihi ukubali kuolewa na mwanaume huyu na khaswa akiwa ni mkubwa kiumri au hata kama wewe unamshinda miaka mitatu. Napenda kumkumbusha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuoa Khadiyjah ilihali yuko na miaka ishirini na tano na yeye Khadiyjah miaka arubaini. Watoto wake wote aliwapata kutoka kwake isipokuwa tu Ibraahiym. Hakuoa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeyote juu yake wakati bado alikuwa yuhai. Alifanya hivo baada ya kufa (Radhiya Allaahu ´anhaa). Namwmabia: ana kiigizo chema kwa Khadiyjah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye ni mama wa waumini. Kijana huyu akiwa ni mtu wa dini na tabia njema, basi amtegemee Allaah na akubali. Desturi zote zinazoenda kinyume na Shari´ah ni batili na hazizingatiwi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (26)
  • Imechapishwa: 21/01/2019