Nasaha juu ya wanandoa kufanya jimaa mchana wa Ramadhaan


Swali: Je, una nasaha zozote juu ya masuala haya  ya kujamiiana mchana wa Ramadhaan[1]?

Jibu: Nasaha zangu ni kwamba kufanya jimaa mchana wa Ramadhaan ndio jambo la khatari na kubwa zaidi linalomfunguza mtu. Ni wajibu kwa mtu kumcha Allaah (´Azza wa Jall). Asiifanye neema ya Allaah kwake kuwa maasi. Allaah amemneemesha mke. Hivyo ni  anapaswa kustarehe naye pale alipomruhusu. Anatakiwa kusubiri. Maambo si mengine isipokuwa ni kusubiri tu masaa machache mpaka jua lizame. Baada ya hapo imehalalika kwake kumwingilia mkewe. Lakini baadhi ya watu wana imani na nafsi dhaifu hawawezi kuzimiliki nafsi zao. Bali utawakuta shaytwaan anawatawala mchana na matamanio yao yanakuwa makubwa zaidi kuliko usiku. Tunamuomba Allaah atupe sisi na wao uongofu.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/mume-na-mke-wameingiliana-mchana-wa-ramadhaan/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/953
  • Imechapishwa: 06/06/2018