Tunamhimidi Allaah kutujaalia sisi na nyinyi kuwa katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba ni neema kubwa; ni neema bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah wangu wote utaingia Peponi isipokuwa yule atayekataa.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni nani atayekataa?” Akasema: “Yule mwenye kunitii ataingia Peponi na atayeniasi atakuwa amekataa.” al-Bukhaariy (7280).

Pindi Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) waliposikia haya walidhania kwamba kuna watu ambao wao wenyewe hawatopenda kuingia Peponi. Kwa ajili hiyo ndipo wakauliza: “Ee Mtume wa Allaah! Ni nani atayekataa?”

Ni nani atayeambiwa ingia Peponi halafu akatae? Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawabainishia makusudio na kusema:

“Yule mwenye kunitii ataingia Peponi na atayeniasi atakuwa amekataa.”

Bi maana mtu ambaye matendo yake mwenyewe yatamzuia na kuingia Peponi. Kushikamana barabara na Sunnah ni sababu kubwa ya kumfanya mtu akaingia Peponi na akasalimika na Moto.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ath-Thabaat ´alaa as-Swiraat al-Mustaqiym yakuun bil-´Ilm http://olamayemen.com/Dars-9998
  • Imechapishwa: 03/05/2018
  • taaliki: umza