Nani ana haki zaidi ya kubaki na mtoto?

Swali: Nani ana haki zaidi ya kuangaliwa na mtoto? Baba au mama?

Jibu: Hakimu ndiye mwenye kuhukumu. Hakimu ndiye anatakiwa kuendewa ikiwa kuna ugomvi kuhusiana na uangalizi wa mtoto. Lakini kwa jumla, na si kwamba nahukumu juu ya suala maalum, mama ndiye mwenye kumuangalia mtoto mpale pale anapofikia umri wa kuweza kupambanua. Anapofikia umri wa kuweza kupambanua basi anaenda kwa baba yake ambaye ndiye anatakiwa kumfunza, kumpa malezi na kumwangalia. Mwanaume ni mwenye nguvu zaidi kuliko mama inapokuja katika malezi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (72) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighassat%20-11-01-1439h.mp3
  • Imechapishwa: 17/12/2017