Swali: Ni ipi kauli yenye nguvu juu ya ni nani alitakiwa kuchinjwa; Ismaa´iyl au Ishaaq?

Jibu: Kauli sahihi ni kwamba alikuwa ni Ismaa´iyl. Baada ya Allaah kutaja kisa chote katika Suurah “as-Swaffaat” akasema:

وَبَشَّرْنَاهُ بِإِسْحَاقَ نَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ

“Tukambashiria Ishaaq – Nabii miongoni mwa waja wema.” (37:112)

Inafahamisha kuwa mchinjwa alikuwa ni Ismaa´iyl. Allaah ameanza kumtaja yeye kwanza pale ambapo Ibraahiym aliposema:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى الْكِبَرِ إِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ الدُّعَاءِ

“Sifa njema na shukurani zote ni za Allaah ambaye amenitunukia juu ya umri mkubwa wangu [watoto wawili] Ismaa’iyl na Ishaaq. Hakika Mola wangu bila shaka ni Mwenye kusikia du’aa yangu.” (14:39)

Allaah kuanza kutaja Ismaa´iyl kabla ya Ishaaq ni dalili yenye kuonesha kuwa yeye ndiye ambaye alikuwa mkubwa kuliko Ishaaq. Hivyo kauli sahihi ni kwamba Ismaa´iyl (´alayhis-Salaam) ndiye ambaye angechinjwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 02/06/2018