Namna ya swalah ya ´iyd kwa ufupi II

Swalah ya ´iyd ni Rak´ah mbili. Imamu atasoma kwa sauti ya juu. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma kwa sauti katika swalah za ´iyd mbili na swalah ya kuomba mvua.”

Ameipokea ad-Daaraqutwniy.

Wanachuoni wameafikiana juu ya hilo na yapo mapokezi ambayo baadhi ya Salaf wameonelea kinyume. Kitendo cha waislamu kiliendelea katika hali hiyo.

Atasoma katika ya kwanza baada ya al-Faatihah atasoma Suurah ”al-A´laa”. Katika Rak´ah ya pili atasoma Suurah ”al-Ghaashiyah”. Samarah amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah za ´iyd mbili alikuwa akisoma:

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

“Tukuza jina la Mola wako Aliye juu.”[1]

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ

“Je, imekujia hadisi ya kufunikiza?”[2]

Ameipokea Ahmad.

Au akisoma katika Rak´ah ya kwanza Suurat ”Qaaf” na ya pili Suurah ”al-Qamar.” Vilevile akisoma mfano wa hizo kwa mujibu wa ilivyopokelewa katika Athar ndio bora zaidi.”

[1] 87:01

[2] 88:01

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mulakhaswsw-ul-Fiqh (01/274)
  • Imechapishwa: 29/07/2020