Namna ya kuziba pengo zinazokuwa baina ya safu

Swali: Je, ni lazima kuziba pengo zilizoko kati ya safu? Ni lazima kuzikutanisha nyayo?

Jibu: Ndio, kuziba pengo ni wajibu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msimwachie pengo/upenyo shaytwaan.”

Shaytwaan hujipenyeza kati ya waswaliji na akawatia wasiwasi. Wakisogeleana na wakaziba pengo shaytwaan hawezi kujipenyeza kati yao. Lakini kuziba pengo haiwi kwa kujipanua na kuchukua nafasi ya watu wawili; kuziba pengo kunakuwa kwa kusogeleana na kuyafanya sawa mabega na visigino.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (92) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20%D9%85%D9%86%20%D9%85%D8%B5%D8%A7%D8%A6%D8%AF%20%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%8A%D8%B7%D8%A7%D9%86-29-07-1439%D9%87%D9%80%200010.mp3
  • Imechapishwa: 25/07/2018