Namna ya kutubu kwa Allaah


Swali: Kuna mtu amerejea kwa Allaah na wala hajui ni vipi atatubu kwa Allaah. Naomba uniwekee wazi hilo.

Jibu: Kurejea kwa Allaah (´Azza wa Jall) ni kule kujutia kwake yale yaliyomtokea, atamani asingetumbukia ndani ya dhambi hiyo na aazimie kutoirudi huko mbeleni. Miongoni mwa sharti hakuna kwamba asiifanye tena. Sharti ni yeye aazimie kutoirudi. Tukikadiria kuwa kuna watu walimpambia nayo na akarudi kufanya maasi hayo, basi tawbah yake ni sahihi juu ya ile dhambi aliyotangulia kufanya. Dhambi hii mpya ni wajibu kuifanyia tawbah nyingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37)
  • Imechapishwa: 24/04/2018