Namna ya kutaamiliana na ndugu anayemtukana Allaah


Swali: Mimi nina ndugu wanaomtukana Allaah (Ta´ala) na mimi ninatangamana nao kama makafiri kwa njia ya kwamba siwatolei Salaam, lakini hata hivyo ninawanasihi kutubu na kuingia upya katika Uislamu. Je, kitendo changu ni sahihi?

Jibu: Ndio, kitendo chako hichi ni wajibu. Ni wajibu kuwalingania katika dini ya Allaah na kuwanasihi huenda wakatubu kwa Allaah. Wewe umetekeleza dhimma na uwajibu wako pale unapowalingania na kuwanasihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13980
  • Imechapishwa: 24/04/2018