Namna ya kuswali swalah ya Istikhaarah na wakati wa kuomba du´aa

Swali: Ni namna gani inaswaliwa swalah ya Istikhaarah? Du´aa inakuwa wakati gani; kabla au baada ya salamu?

Jibu: Swalah ya Istikhaarah imependekezwa. Du´aa inakuwa baada ya salamu, kama ilivyosimulia Hadiyth tukufu.

Namna yake ni kwamba mtu ataswali Rak´ah mbili kama anavyoswali swalah nyenginezo zilizopendekezwa. Atasoma katika kila Rak´ah ufunguzi wa Kitabu na kile kitachomkuia chepesi katika Qur-aan, kisha atanyanyua mikono baada ya salamu na ataomba ile du´aa iliopokelewa juu ya jambo hilo:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ، وَأَسْتَقْدِرُكَ بِقُدْرَتِكَ، وَأَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ العَظِيمِ، فَإِنَّكَ تَقْدِرُ وَلاَ أَقْدِرُ، وَتَعْلَمُ وَلاَ أَعْلَمُ، وَأَنْتَ عَلَّامُ الغُيُوبِ، اللَّهُمَّ إِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ خَيْرٌ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي  فَاقْدُرْهُ لِي، وَيَسِّرْهُ لِي، ثُمَّ بَارِكْ لِي فِيهِ، وَإِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ شَرٌّ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي – أَوْ قَالَ عَاجِلِ وَآجِلِهِ – فَاصْرِفْهُ عَنِّي، وَاصْرِفْنِي عَنْهُ، وَاقْدُرْ لِي الخَيْرَ حَيْثُ كَانَ، ثُمَّ أَرْضِنِي به

”Ee Allaah! Hakika mimi nakutaka ushauri kwa ujuzi Wako na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako na nakuomba kutokana na fadhilah Zako tukufu. Hakika Wewe unaweza, nami siwezi, unajua, nami sijui Nawe ni mjuzi wa yaliyofichikana. Ee Allaah! Iwapo unajua kuwa jambo hili – alitaje kwa jina lake kama ni kuoa, safari au chenginecho – lina kheri nami katika dini yangu, maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi nakuomba uniwezeshe nilipate na unifanyie wepesi kisha unibarikie kwacho. Endapo unajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu, maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi liweke mbali nami, uniepushe nalo na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, halafu niridhishe kwalo.”[1]

Ameipokea Imaam al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

[1] al-Bukhaariy (1096).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/421)
  • Imechapishwa: 14/11/2021