Namna ya kusafisha mkeka/zulia kwa mkojo wa mtoto

Swali: Ni ipi njia ya kusafisha mkeka ambao umekojolewa na mtoto? Ni kiwango kipi cha maji kinachotosheleza kuoga?

Jibu: Mtoto huyu ima akawa wa kiume au wa kike. Akiwa ni mtoto wa kiume mchanga ambaye anakunywa maziwa tu, basi jambo lake ni nyepesi. Kwa sababu twahara ya mtoto wa kiume ambaye bado hajaanza kunywa maziwa inapatikana kwa kumwagilia maji juu yake tu pasi na kusugua. Dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliletewa mtoto wa kiume mchanga ambaye hajaanza kula chakula ambapo akamuweka kwenye mapaja yake na akawa amemkojolea. Akaomba kuletwe maji na akanyunyizia juu yake.

Ama mtoto wa kiume akiwa mkubwa ambaye tayari anatumia chakula au ikawa ni mkojo wa mwanamke, ijapokuwa  atakuwa bado mchanga, kinachotakiwa kufanywa kwanza ni kuondosha ule mkojo,  halafu kunyunyiziwe juu yake maji kisha maji yale yaondoshwe/kukamuliwa. Halafu kunyunyiziwe juu yake maji tena kisha maji yale yaondoshwe/kukamuliwa. Halafu mtu anyunyizie mara ya tatu na hapo itatosha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1043
  • Imechapishwa: 04/03/2019