Namna ya kurudisha wasiwasi wa shaytwaan ndani ya swalah

Swali: Ni vipi tutarudisha wasiwasi ndani ya swalah?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwelekeza ´Uthmaan bin Abiy al-´Aasw wakati alipomweleza kwamba shaytwaan anamtatiza katika swalah yake ambapo akamwambia:

“Tema cheche za mate kushotoni mwako na umtake Allaah kinga dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa.”

Kwa hivyo mtu anatakiwa kutema cheche za mate khafifu na amtake Allaah kinga dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa. ´Uthmaan amesema kuwa aliyatendea kazi hayo na Allaah akamwondoshea yale aliyokuwa akihisi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 17/04/2019