Namna ya kupanga safu msikiti ukiwa mfinyo

Swali: Sisi tuna mahali pa kuswalia (Muswallaa) masomoni na kumejibana kwa waswaliji kiasi cha kwamba baadhi ya waswaliji wanaswali pamoja na imamu katika safu ya kwanza. Je, bora imamu abaki katikati na maamuma waswali upande wa kulia na wa kushoto kwkae au bora imamu aswali upande wa kushoto na maamuma wengine wote wawe upande wa kuliani mwake?

Jibu: Mahali pakiwa ni penye kujibana kiasi cha kwamba imamu hawezi kutangulia mbele na maamuma wakaswali nyuma yake, basi lililo bora imamu aswali katikati yao. Kwa mfano ni watatu basi mmoja wao aswali upande wake wa kulia na mwingine aswali upande wake wa kushoto. Hali ilikuwa namna hii mwanzoni mwa Uislamu. Watu watatu walikuwa wakiswali safu moja na imamu akiwa katikati yao. Kisha baadaye likafutwa na ikawa wakiwa watu ni watatu basi imamu anatangulia mbele. Haitakiwi wawe upande wake wa kuume tu, kama wanavyofahamu baadhi ya wasiokuwa na elimu. Akiwa imamu na mswaliji ni mmoja atasimama wapi? Atasimama upande wa kulia. Kwa sababu katika hali hii jambo linapelekea ima awe upande wa kulia au wa kushoto. Tunasema upande wa kulia ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (69) http://binothaimeen.net/content/1558
  • Imechapishwa: 28/02/2020