Namna ya kuosha najisi ilioshika kwenye mkeka

Swali: Najisi ikiingia kwenye mkeka na najisi hii ikawa kubwa na najisi hii ikawa sehemu yake tu, ni wajibu kuosha mkeka wote?

Jibu: Mtu aoshe pale palipopatwa na najisi ikiwa kumejulikana. Au mtu aoshe pale ambapo anadhani na ana dhana yenye nguvu kwamba kumepatwa na najisi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 25/09/2018