Swali: Nikimuona baba yangu anatazama dishi ni nasaha zipi niwezazo kumpa ili nisimuasi na wala kumpaka mafuta?

Jibu: Nasaha ni kufanya upole kwake na kutafuta wakati ambapo kifua chake kinakuwa ni chenye kufunguka na uzungumze nae kwa siri mara baada ya nyingine. Ukifanikiwa, umefikia lengo, usipofanikiwa, basi hakuna neno kumuwea uwazi mambo na kuzungumza nae waziwazi kama alivyofanya Ibraahiym (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) pindi alipokuwa anazungumza na baba yake:

يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا

“Ee baba yangu! Kwa nini unaabudu vile visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa kitu chochote?” (19:42)

يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا

“Ee baba yangu! Hakika mimi imekwishanijia elimu isiyokufikia wewe, hivyo basi nifuate nikuongoze njia iliyonyooka.” (19:43)

Anamwamrisha baba yake amfuate kwa sababu amejiwa na elimu ambayo haikumfikia yeye:

يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ عَصِيًّا يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا

“Ee baba yangu! Usimuabudu shaytwaan, kwani hakika shaytwaan kwa Mwingi wa rehema daima ni muasi. Ee baba yangu! Hakika mimi nachelea kukushika adhabu kutoka kwa Mwingi wa rehema utakuja kuwa rafiki kwa shaytwaan.” (19:44-45)

Muhimu ni kwamba lililo la wajibu ni yeye kuongea kwa uzuri na baba yake na amwamrishe mema na kukataza maovu kwa njia ya karibu ambayo anaweza kwayo kufikia malengo. Hata hivyo hatakiwi kukata tamaa. Baadhi ya watu pindi baba yake anapohamaki au kumtukana basi anaacha. Hili ni kosa. Unachotakiwa ni wewe kuwa na subira, vuta subira, baki imara na wala usikate tamaa. Lakini hata hivyo mambo kati yako wewe na yeye yanatakiwa kubaki siri. Hapo ndipo atakuwa karibu zaidi na kukubali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/774
  • Imechapishwa: 03/12/2017