Swali: Mtu ambaye ana kafara nyingi za kiapo anakafiria kwa kila kiapo kimoja au inatosha kwake kuwalisha masikini kumi mara moja?

Jibu: Inategemea. Ikiwa kiapo kimekariri na kimetolewa kwa mara moja basi atakafiria kafara moja. Ama ikiwa ni viapo vingi basi itabidi atoe kafara nyingi. Kwa mfano akiapa kwa Allaah kwamba hatokula chakula cha fulani mara tatu, itamlazimu atoe kafara moja. Kwa sababu ameitoa kwa aina moja. Lakini akisema kwa kukusudia na akaapa kwa Allaah kwamba hatokula chakula cha fulani, kwamba hatoingia nyumbani kwake na kwamba hatomzungumzisha, hapa kuna viapo vitatu. Itambidi atoe kafara kwa ajili ya kula, kuzungumza na kuingia nyumbani kwa mtu huyo. Katika hali hii ni lazima awalishe masikini kumi na hawatoshi masikini sita. Kwa sababu Allaah amesema:

فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ

“Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi… “[1]

Vilevile anaweza kuwalisha. Akipata wanafamilia sita basi anaweza kuwalisha kisha akatafuta wengine wane ili aweze kukamilisha idadi ya watu kumi. Kiapo kingine afanye vivyo hivyo kulisha masikini kumi.

[1] 05:89

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 01/12/2018