Namna ya kujibu salamu ya kafiri

Swali: Akikujia kafiri na akaanza kukutolea salamu. Je, inafaa kumrudishia kwa kusema “wa ´alayakas-Salaam”? Ni vipi mtu amjibu? Je, inajuzu kwa mtu kuanza kumtolea salamu? Ni yepi maoni yako?

Jibu: Haijuzu kuanza kumtolea kafiri salamu kwa kumwambia: “as-Salaam ´alaykum”. Lakini akitutolea salamu basi mjibu kwa tamko lifuatalo “wa ´alayakum”. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndivo kaamrisha inapokuja kwa mayahudi na manaswara. Mbali na hawa wana hukumu moja kama wao kama wao watakuwa sio duni kuliko wao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (01) http://binothaimeen.net/content/6628
  • Imechapishwa: 01/02/2019