Swali: Ni vipi nitafaidika kwa kusoma vitabu vya elimu ili visipotee bure?

Jibu: Mosi: Watu wanatofautiana katika jambo hili. Baadhi ya watu wanakuwa hifdhi yenye nguvu na werevu. Wanahifadhi kitabu kwa kule kukipitia mara moja tu na wanafahamu pia maana. Wengine wana hifdhi lakini hawana werevu. Wengine wana werevu na hawana hifdhi. Lakini yule mwenye upungufu anatakiwa kufanya mapambano kujikamilisha kwa kurejearejea kwa wingi. Miongoni mwa mambo bora kabisa ni wewe ukadirie kwa mfano kuhifadhi misitari mitano. Ikariri mpaka iwe kwako kama vile unavyosoma al-Faatihah. Kisha baada ya hapo unaenda sehemu nyingine. Halafu unarejelea yale uliyosoma jana.

Nataka nielezee yale niliyokuwa nafanya: nilikuwa nahifadhi matini alasiri. Asubuhi narejelea na hivyo najikuta nimeyahifadhi. Baadhi ya watu wengine wanasema wanafanya kinyume na hivyo; wanahifadhi mwanzoni mwa mchana na wanarejelea mwishoni mwa mchana na hivyo wanajikuta wamehifadhi. Mtu ndiye kiongozi wa nafsi yake mwenyewe.

Pili: Unapopitia faida tukufu basi iandike. Tenga daftari maalum kwa ajili ya kuandika masuala haya. Kwa ajili imesemwa:

“Ifungamanishe elimu na uandishi.”

Tatu: Pupia kufanya utafiti pamoja na marafiki zako na mwishoni jambo liishilie kwa Shaykh. Kwa sababu kwa kufanya utafiti akili inafunguka zaidi na mtu anajizoweza juu ya mjadala. Sisi hii leo tunahitajia watu wenye kujua kujadili vizuri. Kwa sababu waovu na watenda madhambi wana ubainifu wenye nguvu na ufaswaha kiasi cha kwamba haki inaweza kupotea kwa sababu ya ubatilifu wao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (67) http://binothaimeen.net/content/1512
  • Imechapishwa: 08/02/2020