Mwanzoni watu wengi walidanganyika na Jamaa´at-ut-Tabliygh na walikuja huku kwetu na tukasema kwamba sisi hatuwaoni isipokuwa ni walinganizi. Hatukuzijua Bid´ah zao isipokuwa baada ya hapo kupitia maneno yao, vitendo vyao na ujinga wao. Mwanzoni Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) alikuwa akiwasifu na kusema kwamba wana bidii na uchangamfu. Lakini baada ya hapo yeye mwenyewe aliwakataza watu kutoka nao isipokuwa mtu ambaye ana elimu na anaweza kuwafunza. Lakini tatizo wao hawamkubalii mtu kuwafunza kwa njia ya kwamba awaamrishe, awakataze na awaelekeze. Ni lazima afuate mwenendo wao. Vinginevyo hutofuatana nao.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah (03)
  • Imechapishwa: 20/05/2019