Namna mchawi na mlaji ribaa watavyojinasua na pesa yao baada ya kutubia

Swali: Mchawi akitubia baada ya kuwa ameshachuma mali kutokana na chumo la uchawi vipi atajinasua nazo khaswa ikiwa mali hii amejenga nayo nyumba au amefanya biashara?

Jibu: Mchawi akitubu tawbah ya kweli kabla ya kudhibitiwa ambapo akatubia na akaachana na jambo hili na akalazimiana na kumtii Allaah (´Azza wa Jall), basi ile mali ya haramu alionayo aitoe swadaqah na kuiweka katika miradi ya kijamii kwa ajili ya kujikwamua nayo. Ni kama mfano wa mlaji ribaa ambaye ana faida za kiribaa kisha baadaye akatubu kwa Allaah na akaacha ribaa. Huyu anatakiwa kuziweka pesa hizi katika miradi ya kijamii ya kuwasaidia watu kwa lengo la kujinasua nazo. Vilevile anaweza kuzitoa swadaqah kuwapa wahitaji.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (07) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 11/01/2019