Namna inavyothibiti Ramadhaan


Swali: Kuingia kwa mwezi wa Ramadhaan kunathibitishwa kwa kitu gani?

Jibu: Kuingia kwa mwezi wa Ramadhaan kunathibitishwa ima kwa kuonekana mwezi au kwa kukamilisha Sha?baan siku thelathini. Mtume (Swalla Allaahu ?alayhi wa sallam) amesema:

“Mkiuona fungeni na mkiuona fungueni. Mkifunikwa na mawingu basi timizeni idadi ya Sha?baan thelathini.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/36)
  • Imechapishwa: 27/05/2017