Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa kivazi kinachovuka kongo mbili za miguu?

Jibu: Kuvaa kivazi kinachovuka kongo mbili za miguu ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kilichoko chini ya kongo mbili za miguu ni Motoni.”

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

Kilichoko chini ya kongo mbili za miguu kitaingia Motoni. Imekuja katika Hadiyth nyengine:

“Atakayeiburuta nguo yake kwa kiburi Allaah hatomtazama.”

Haya ni makemeo makali. Akiiburuta nguo yake kwa majivuno Allaah hatomtazama. Akiivaa pasi na kiburi itaunguzwa na Moto. Katika Hadiyth nyingine iliyoko katika “as-Swahiyh” ya Muslim:

“Kuna watu aina tatu ambao Allaah hatowazungumzisha, Allaah hatowatazama siku ya Qiyaamah na wala hatowatakasa na watakuwa na adhabu yenye kuumiza; mwenye kuburuta izari yake, mwenye kuuza bidhaa yake kwa viapo vya uongo na mwenye kueneza uvumi.”

Mwenye kuburuta izari yake ni yule mwenye kuvaa nguo yake ikapita chini ya tindi mbili za miguu. Ni mamoja nguo hiyo ni kanzu, suruwali na jinzi. Haijuzu kuyateremsha mavazi haya chini ya kongo mbili. Ni wajibu yawe juu ya kongo mbili za miguu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=67941&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 29/07/2017