Namna hii ndivo anaheshimiwa Mtume

Swali:  Ni ipi hukumu ya kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mwezi wa Rabiy´ al-Awwal kwa lengo la kumuadhimisha (´alayhis-Swalaatu was-Salaam)?

Jibu: Kumuadhimisha Mtume na kumheshimu inakuwa kwa kuamini yale yote aliyokuja nayo kutoka kwa Allaah na kufuata Shari´ah yake sawa katika ´Aqiydah, maneno, matendo na tabia na sambamba na hilo mtu akaacha kuzusha katika dini. Miongoni mwa mambo yaliyozuliwa katika dini ni kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz ana maneno yenye kutosheleza amezungumzia hukumu ya kusherehekea Maulidi ya Mtume[1].

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kuhusu-kusherehekea-maulidi/

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/13-14)
  • Imechapishwa: 22/08/2020