Namna hii ndio utapambanua mlinganizi wa Sunnah na Bid´ah

Swali: Vipi tutajua ni nani anayelingania katika Sunnah na anayelingania katika Bid´ah?

Jibu: Kwa kutazama yale wanayolingania kwayo. Ikiwa wanalingania katika Sunnah na katika madhehebu ya Salaf-us-Swaalih na Ahl-us-Sunnah na wameshikamana na mfumo sahihi, itakuwa ni wa kweli katika ulinganizi wao.

Ama ikiwa wanaita harakati zao “ulinganizi katika dini ya Allaah” na wanaeneza fikira zinazoenda kinyume na dini ya Allaah, hawa ni walinganizi wa upotevu. Ni lazima kwa mtu kutahadhari nao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: at-Tahdhiyr min Du´aat-is-Suu’
  • Imechapishwa: 05/09/2020