Namna hii Haddaadiyyah wanaenda kinyume na maafikiano ya Salaf

Ahl-us-Sunnah wanawapiga vita Murji-ah na wamesema kabla hamjazaliwa ya kwamba imani ni maneno na vitendo, inapanda kwa matendo mema na inashuka kwa maasi. Ndio ´Aqiydah wanayoafikiana kwayo Maswahabah, Taabi´uun na Ahl-us-Sunnah wengine wote katika zama zote mpaka hii leo.

Nyinyi, Haddaadiyyah wajinga na wenye kudhulumu, hamridhiki na taarifu hii iliyoafikiwa kwayo kwa kuwa mnawadharau na kuwapuuza Salaf na elimu yao. Lau mngeliyapima maneno yao basi msingewapita. Katika maana ya imani mmeongeza kwa kushurutisha ya kwamba inashuka mpaka hakubaki chochote katika imani. Baada ya hapo mkawatuhumu wale wasiotaja nyongeza hiyo upotevu na Irjaa´. Sharti yenu inapelekea kuwafanyia Tabdiy´ Salaf na kuvunja maafikiano yao. Hii ni Bid´ah kubwa na ni fitina kubwa. Kwa sababu ya ujinga wenu na uchafu wenu hamuoni kuwa hii ni Bid´ah na ina maana gani.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 34
  • Imechapishwa: 09/10/2016