Swali: Je, ni katika Sunnah mfungaji wakati anakata swawm akala baadhi ya tende na akanywa maji kisha akasimama kuswali Maghrib halafu baada ya hapo ndio akala na kunywa akitakacho?

Jibu: Ndio, kwa sababu akifanya hivo ndio anaweza kukusanya kati ya manufaa. Aharakie futari katika vile ambavyo Allaah amemrahisishia katika tende tosa, tende za kawaida au maji. Baada ya hapo aende kuswali swalah ya mkusanyiko ili asikose swalah ya mkusanyiko. Kisha atarejea na kula chakula cha jioni. Kufanya hivi ndio sawa.

Lakini kwa mfano kama watakuwa kundi la watu safarini basi inafaa kwao kukata swawm, kisha wale chakula cha jioni halafu waswali. Endapo watachelewesha chakula cha jioni, wakatanguliza swalah baada ya kukata swawm hapana vibaya. Ama katika miji mikuu na vijiji watu wanatakiwa kutumia vile ambavo Allaah amewarahisishia katika futari kisha baada ya hapo waende kuswali ili wasikose swalah ya mkusanyiko.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12020/كيفية-الجمع-بين-الافطار-وصلاة-المغرب
  • Imechapishwa: 18/04/2022