Namna Allaah anavyowafanyia vitimbi makafiri

Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّـهُ

”Wanapanga vitimbi na Allaah anapanga vitimbi.” (08:30)

Ni vipi Allaah anawafanyia vitimbi makafiri?

Jibu: Namna Allaah anawafanya vitimbi makafiri amelitaja hilo pale aliposema:

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ

”Wale waliokadhibisha Aayah Zetu Tutawavuta polepole kwa namna wasiyoijua. Nitawapa muhula – hakika njama Zangu ni zenye nguvu.” (07:182-183)

Hivi ndivyo Allaah huwafanyia vitimbi maadui wake. Allaah huwavuta polepole na kuwafanyia wepesi sababu za kuyaendea maasi na kufuru mpaka hatimae wakaendelea katika kufuru yao na wakafa juu ya hilo. Hivi ndizo njama zenyewe.

Kwa hivyo hapa tunapata kujua ya kwamba Allaah akimpa majaribio muumini kwa mtihani basi hiyo ni neema juu yake. Kwa hayo Allaah (Ta´ala) anamsamehe madhambi yake, kuuzindua moyo wake na anapata kujua kuwa amekosea na matokeo yake ananyooka. Lakini upande mwingine wale waliokufuru wanaharakishiwa mazuri katika maisha yao haya ya duniani na watakuja kupata khasara siku ya Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (30) http://binothaimeen.net/content/680
  • Imechapishwa: 18/10/2017