Swali: Je, kilemba kinapanguswa mara moja au ni kama kichwa; kuanzia maoteo ya kichwa kwenda shingo na kurudi?

Jibu: Ni kama kichwa; anaanzia kwenye maoteo ya nywele na kupangusa na mikono kwenda kwenye shingo kisha arudi kwenda ile sehemu aliyoanzia. Haijalishi kitu sawa ikiwa atapangusa kichwa au kilemba. Ibn-ul-Qayyim amesema kuwa kuna sifa tatu za kupangusa kichwa:

1- Mtu apanguse sehemu inayoonekana ya mbele ya kichwa na sehemu iliobaki ya kilemba.

2- Ikiwa kilemba kinafunika kichwa kizima mtu apanguse kilemba kizima.

3- Ikiwa hana kilemba apanguse moja kwa moja kichwani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsirayat-12-07-1435-01_0.mp3
  • Imechapishwa: 18/05/2018