Najisi ya nguruwe si kama najisi ya mbwa

Mbwa akiramba chombo basi kinatakiwa kuoshwa mara saba ambapo osho moja liwe kwa mchanga, kama ilivyothibiti katika Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wako wanachuoni ambao wametumia kipimo cha mbwa juu ya nguruwe, kipimo ambacho si sahihi. Kwa sababu Allaah amezumgumzia nguruwe ndani ya Qur-aan na anatambulika. Pamoja na hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumfanya kuwa na hukumu moja kama ya mbwa. Kila kitu ambacho sababu yake ilikuweko wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lakini hata hivyo asihukumu kwa kitu, basi haitosihi kuhukumu juu yake kwa kitu kinachokwenda kinyume na yale waliyokuwemo katika zama zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kujengea juu ya haya ni kwamba najisi ya nguruwe ni kama najisi nyenginezo. Ina maana kwamba akiramba ndani ya chombo hakitooshwa mara saba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Vrcg5Aoyyug
  • Imechapishwa: 04/10/2020