Najisi Ilio Kwenye Nguo Au Mwili Hailazimishi Kutawadha Upya

Swali: Wakati wa swalah mswaliji amekumbuka kuwa kuna najisi kwenye nguo zake na akawa ameosha najisi hii. Je, ni lazima kwake kurudi kutawadha upya?

Jibu: Hapana. Najisi iliyo kwenye nguo na mwilini inaondoshwa na wala wudhuu´ haurudiliwi. Hakutawadhiwi kwa sababu ya najisi. Wudhuu´ ni kitu kimoja na najisi ni kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (9) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340506.mp3
  • Imechapishwa: 14/04/2017