Naibu hajj ana thawabu sawa na yule anayemuhijia?

Swali: Ambaye amewakilishwa kumuhijia mtu mwingine anafikiwa na yale aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayefanya hajj kisha asiseme maneno machafu na wala asitende matendo machafu, basi atarudi akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake.”?

Jibu: Swali hili linakomeka kwa sisi kuuliza: je, mtu huyu amehiji? Hakuhiji. Amemuhijia mwingine na hakujihijia yeye mwenyewe. Hivyo hapati thawabu alizosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu uhakika wa mambo ni kwamba hakujihijia yeye mwenyewe. Bali amemuhijia mwingine. Lakini – Allaah akitaka – akikusudia kumnufaisha nduguye na kumkidhia haja yake, basi Allaah atamlipa thawabu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/972
  • Imechapishwa: 20/12/2018