Nafsi ya Allaah ina maana ya dhati?

Swali: Maneno ya Allaah (Ta´ala):

تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ

“Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala mimi sijui yale yaliyomo katika nafsi Yako.” (05:116)

Je, hapa kuna kuthibitisha Nafsi kwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala)?

Jibu: Ndio, bila ya shaka. Allaah anathibitishiwa kuwa na nafsi:

وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ

“Na Allaah Anakutahadharisheni nafsi Yake.” (03:30)

تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ

“Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala mimi sijui yale yaliyomo katika nafsi Yako.” (05:116)

Lakini hata hivyo sio kama nafsi za viumbe. Nafsi Yake ni kama mfano wa Sifa Zake zingine zote (Subhanaahu wa Ta´ala).

Swali: Je, ifasiriwe kuwa ni dhati?

Jibu: Hapana, isifasiriwe hivyo. Ifasiriwe kama ilivyokuja. Ni nafsi ya Allaah isiyofanana na nafsi za viumbe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (14) http://alfawzan.af.org.sa/node/2118
  • Imechapishwa: 05/07/2020