Nafsi inatakiwa kuifanyiwa hesabu kila wakati, na si mwisho wa mwaka tu


Swali: Ni jambo limekithiri siku hizi kufikiri na kuifanyia hesabu nafsi inapofika mwisho wa mwaka. Je, kitendo hichi kina msingi katika Shari´ah?

Jibu: Jambo la kuifanyia hesabu nafsi linakuwa katika kila wakati. Inatakiwa kwa watoa mawaidha na walinganizi kuwakumbusha watu wazifanyie hesabu nafsi zao kila wakati.

Ama kuifanyia nafsi hesabu mwishoni mwa mwaka ni jambo la mnasaba. Ama kusema kuwa ni jambo lina msingi katika Qur-aan na Sunnah sijui hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 03/01/2018