Nadhiri ya kufunga mwezi mzima akipata mume

Swali: Niliweka nadhiri ya kufunga mwezi mzima Allaah akinijaaliwa kuolewa. Namshukuru Allaah nimeolewa. Je, nalazimika kufunga? Nifanye nini kama siwezi?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ambaye ameweka nadhiri ya kumtii Allaah basi na amtii.”

Allaah (Ta´ala) amesema juu ya waumini:

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا

“Wale ambao wanatimiza nadhiri zao na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea.” (76:07)

Ukiweka nadhiri ya utiifu, kama hiyo nadhiri uliyoweka ya kufunga mwezi mzima ukiolewa, hii ni nadhiri ya utiifu na umepata mume hivyo mshukuru Allaah. Unatakiwa kufunga mwezi mzima na wala huna udhuru muda wa kuwa unaweza.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-13-11-1435هـ-0
  • Imechapishwa: 19/06/2022