Swali: Ni lazima kulipa swawm ya nadhiri kabla ya kuanza kulipa mwezi wa Ramadhaan au si lazima? Ikiwa ni lazima juu yake mtu huyu atakuwa na nini ikiwa kama ataanza kufunga Ramadhaan kwanza?

Jibu: Lililo wajibu kwa ambaye ameweka nadhiri iliofungamana na sharti basi aitimize pale tu kutapopatikana sharti hiyo. Hatakiwi kuchelewesha. Mfano wa hilo mtu akaweka nadhiri ya kufunga siku tatu pindipo tu Allaah atapomponyesha maradhi yake. Baada yake akaponya na maradhi hayo. Hivyo ni wajibu kwa mtu kuharakisha kufunga siku hizi na asicheleweshe. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللَّـهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ فَلَمَّا آتَاهُم مِّن فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ وَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ

”Na miongoni mwao wako waliomuahidi Allaah kwamba akitupa katika fadhilah Zake, basi hakika tutatoa swadaqah na tutakuwa miongoni mwa waja wema. Alipowapa katika fadhilah Zake, walizifanyia ubakhili na wakakengeuka ilihali ni wenye kupuuza. Basi akawaadhibu kwa unafiki katika nyoyo zao mpaka siku watakayokutana Naye kutokana na yale walivyomkhalifu kwao Allaah kwa waliyomuahidi na kutokana na yale waliyokuwa wakikadhibisha.”[1]

Kuhusu nadhiri ambayo haikufungamana na sharti yoyote, kwa mfano mtu akaweka nadhiri ya kuwajiwajibishia kufunga siku tatu kwa ajili ya Allaah pasi na sababu yoyote. Katika hali hii ni wajibu kwa mtu huyu kuharakisha. Lakini sio kama ile hali ya kwanza. Ramadhaan ikimfikia ilihali bado hajafunga, ni jambo linalotambulika kwamba anatakiwa kuanza Ramadhaan. Ramadhaan itapomaliza ndipo anatakiwa kufunga nadhiri. Lakini iwapo atafunga nadhiri yake katika Ramadhaan, basi haitosihi swawm ya nadhiri yake wala swawm ya Ramadhaan.

Mtu anadaiwa kufunga nadhiri siku tatu ambapo akafunga siku tatu za Ramadhaan kwa kunuia nadhiri. Kipi kinachomuwajibikia? Swawm yake ya nadhiri haimfai kitu wala ya Ramadhaan. Kule swawm yake ya nadhiri kutomfaa kitu ni kwa sababu Ramadhaan wakati wake ni mfinyu. Si sahihi kufunga swawm nyingine ndani yake. Kule kutomtosheleza kwake na Ramadhaan ni kwa sababu hakunuia kufunga Ramadhaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila matendo yanategemea nia na kila mmoja atalipwa kwa lile alilonuia.”

[1] 09:75-77

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (52) http://binothaimeen.net/content/1173
  • Imechapishwa: 14/06/2020