Nadharia ya Mufawwidhwah ni mbaya zaidi kuliko ya makafiri

Imesimuliwa kutoka kwa baadhi ya watu wajinga wakiuliza ni vipi mbingu zinakuwa wakati Allaah anaposhuka. Wakasema:

“Huzinyanyua kisha huzishusha. Yeye ni muweza wa kufanya hivo.”

Kila ambaye anafikiria yale ambayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemsifu Mola wake ni kama sifa za viwiliwili vyao ni wenye kupotea. Kisha baada ya hapo wanajigawanya makundi mawili.

Kundi la kwanza limesema kuwa ufahamu huo ni batili. Wameamini kuwa ufahamu ni ule uliofahamishwa na udhahiri wa maandiko na kwamba mtu hawezi kuyafahamu kwa njia nyingine mbali na hiyo. Hayo yakawafanya ima kukengeusha makengeusho yenye maana ya kuyaondosha maneno kutoka mahala pale stahiki au kusema kwamba mtu hafahamu chochote kwa maandiko hayo.  Wanasema kuwa haya ndio madhehebu ya Salaf. Wanafasiri maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ

“Hakuna ajuae tafsiri zake isipokuwa Allaah.”[1]

na kusema kwamba Allaah pekee ndiye anajua maana ya zile Aayah zisizokuwa wazi maana yake. Vilevile wanasema kuwa maana ya Hadiyth haziko wazi na kwamba Hadiyth zinazozungumzia kuhusu kushuka kwa Allaah haziko wazi maana yake. Hayo yanapelekea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye ndiye katamka Hadiyth kuhusu kushuka kwa Allaah alikuwa hajui anachokisema wala alichokuwa anamaanisha kwa maneno yake. Hivi kweli inafaa kwa mtu mwenye akili kufikiria hivi, sembuse tusisemi Mitume, sembuse tusisemi mtu mbora wa mwanzo na wa mwisho, kiumbe ambaye ndiye mjuzi zaidi, mfaswaha zaidi na mwenye kuwatakia watu kheri zaidi?

Pamoja na haya yote wanadai kuwa wao ni Ahl-us-Sunnah na kwamba maoni haya wanayomsifu kwayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Ummah wake ndio maoni ya Ahl-us-Sunnah. Hapana shaka kwamba hawakufikiria uhakika wa kile walichokisema, lau wangelizingatia basi wangeliona kuwa maoni yao yanapelekea katika yaliyo mabaya zaidi kuliko yale ambayo makafiri walisema kuhusu Mitume. Wao wenyewe hawako radhi juu ya yule mwenye kumponda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanaona kuwa ni halali kumuua yule mwenye kumponda. Ni wenye kupatia pale wanapoonelea kufaa kuuliwa yule mwenye kuwaponda Mitume (´alahis-Salaam). Hata hivyo maoni yao yanapelekea katika matusi makubwa zaidi. Lakini hawayajui hayo na yale yanayopelekea katika maoni fulani sio maoni.

[1] 03:07

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 113
  • Imechapishwa: 04/04/2019