Swali: Mwaka uliopita nilisoma kitabu cha historia namna ambavyo mtu ametokamana na nyani na muda ulivokuwa unaenda akawa mtu. Je, haya ni kweli au yanapingana na yale yaliyomo ndani ya Qur-aan juu ya chimbuko la nyani?

Jibu: Si kweli kwamba msingi wa mtu anatokamana na nyani. Hata hivyo ukweli wa mambo mtu aliyesema hivo yeye ndiye ngedere. Amefutwa akili na uoni. Yeye ndiye anastahiki kuitwa nyani na si mtu ingawa atakuwa anafanana na mtu.

Swali: Je, ni sahihi kusema kuwa amegeuka kuwa nyani kikweli kwa sababu Freud alikuwa myahudi?

Jibu: Yale niliyosema mimi ndio bora. Niliyosema yanatosha. Nadharia hii kwamba msingi wa mtu anatokamana na nyani si sahihi. Kuamimi hivo ni ukafiri kwa sababu ni kuikadhibisha Qur-aan. Allaah (Ta´ala) amebainisha kwamba mtu amemuumba kutokamana na udongo kwa kumuumba Aadam (´alayhis-Salaam). Yeye ndiye baba wa watu. Kisha akajaalia kizazi chake kutokana na mchujo safi wa maji dhalilifu. Nyani wanaotambulika ni miongoni mwa viumbe wengine. Wametokana kwa njia ya maumbile ya kawaida. Allaah (Ta´aal) amewaumba kwa umbile lao kama Alivyowaumba punda, mijibwa, nyumbu, farasi, ngamia, ng´ombe, kondoo, swala, kuku na wengineo. Haijuzu kwa yeyote wala nchi ya Kiislamu kufunza jambo hilo katika masomo yao. Ni lazima kufuta jambo hilo kutoka kwenye masomo yao. Kwa sababu mwanafunzi anapojifunza hivo kuanzia utotoni mwake inakuwa ni vigumu sana kumwondosha fikira hiyo baada ya kuwa mkubwa. Sionelei kuwa inafaa kufunza fikira hii hata kama ni kwa lengo la kuirudisha. Ni maharibifu. Bora ni kutoisoma kabisa kuliko kuisoma kisha ikarudiwa.

Ni lazima kwa nchi za Kiislamu kuchunguza vizuri silebasi zao na kuzijenga juu ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili Allaah aweze kurudisha juu ya Ummah wa Kiislamu utukufu wake, nguvu zake na heshima yake na kuwaondoshea udhalilifu ambao mpaka maadui zao wanawasikitikia. Adui anawaonea huruma kutokana na ule mpasuko, mtengano, udhalilifu na unyonge uliowapata. Ni jambo ambalo hali halisi ya mambo inashuhudia hilo. Hali hiyo inatokana na wengi wao kupuuzilia mbali Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na njia ya Salaf ambayo Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema juu yake:

“Hautotengemaa mwisho wa Ummah huu isipokuwa kwa yale yaliyofanya wa mwanzo wao kutengemaa.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (55 A)
  • Imechapishwa: 17/06/2021