Nadharia inayosema kuwa kabla ya Aadam walikuwepo viumbe wengine

Swali: Kipindi cha mwisho kumedhihiri kwenye TV watu ambao kunasemwa kwamba ni Fuqahaa´ na wanachuoni ambao wanasema kuwa Aadam (´alayhis-Salaam) sio kiumbe cha kwanza na kwamba kuna viumbe waliokuwa kabla yake. Lakini hata hivyo Allaah aliwafadhilisha juu yao. Vilevile wanasema kwamba Aadam ana baba na mama na kwamba Hawwaa hakuumbwa kutoka kwenye ubavu wa Aadam. Unasemaje juu ya hili?

Jibu: Hii ni kufuru. Hii ni kufuru na ukanajimungu. Ni kupingana na maneno Yake  (Jalla wa ´Alaa) yanayosema kwamba Allaah amemuuba Aadam kutokamana na udongo, amemuumba kwa mikono Yake na kwamba hana baba wala mama. Vilevile ni kupingana na kwamba amemuumba Hawwaa kutokamana na yeye Aadam. Mwenye kukanusha haya anakuwa ni mwenye kumkufuru Allaah (Jalla wa ´Alaa) na anaritadi katika Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 08/12/2017