241- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakukuwa Nabii yeyote kabla yangu isipokuwa ilikuwa ni wajibu kwake kuwaelekeza Ummah wake katika yale ambayo anajua ni kheri kwao na kuwatahadharisha na yale ambayo anajua ni shari kwao. Ummah wenu umefanyiwa usalama wao kuwa mwanzoni mwake. Mwishoni mwake utapatwa na mitihani na mambo msiyoyatambua. Mitihani itajitokeza na kuvutana yenyewe kwa yenyewe. Mtihani utajitokeza ambapo muumini atasema: “Hapa ndio kuangamia kwangu.” Baadaye uishe. Kisha ujitokeze mtihani mwingine aseme: “Huu sasa huu sasa.” Yule anayetaka kuokolewa na Moto na kuingia Peponi basi kimjie kifo chake ilihali anamwamini Allaah na siku ya Mwisho na atangamane na watu vile anavyopenda watu watangamane naye. Yule atakayekula kiapo cha utiifu kwa kiongozi na akampa mkono wake na matunda ya moyo wake, basi amtii kiasi na anavyoweza. Atapokuja mwingine kukizana naye basi likateni shingo la huyo mwingine.”

Ameipokea Muslim (6/18), an-Nasaa’iy (2/185), Ibn Maajah (2/466) na Ahmad (2/191) kupitia njia nyingi kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Zayd bin Wahb, kutoka kwa ´Abdur-Rahmân bin ´Abdi Rabb-il-Ka´bah.

Katika Hadiyth kuna faida nyingi. Moja amabyo ni muhimu zaidi ni kwamba ni lazima kwa Nabii kuwalingania Ummah wake katika kheri na kuwaelekeza kwayo na kuwatahadharisha yale anayojua ni shari kwao. Ndani ya Hadiyth kuna Radd ya wazi juu ya yale maoni yanayosema kuwa Nabii ni yule ambaye anateremshiwa Wahy na haamrishwi kufikisha, kama ilivyo katika baadhi ya vitabu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/1/486)
  • Imechapishwa: 20/05/2019