Swali: Mwenye kuhuisha njia mbaya kisha akafuatwa na watu. Baadaye mtu huyo akatubia lakini watu wakaendelea kumfuata. Je, atapata dhambi?

Jibu: Udhahiri ni kwamba akitubu tawbah ya kweli basi hakuna juu yake kitu. Isipokuwa ikiwa wako karibukaribu na anaweza kuwafikishia. Katika hali hiyo ni lazima kuwafikishia ili wasimwigilize. Lakini asipoweza kuwafikishia basi nataraji kuwa kule kutubu kwake kunatosha. Shirki ni kubwa zaidi kuliko hayo. Lakini kama anaweza kupata anwani zao au wakawa karibukaribu basi analazimika kuwafikishia kwamba amekosea katika jambo hilo na amejirejea kutokamana na kosa hilo ili wasije kumwigiliza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21531/حكم-من-سن-سنة-سيىة-وتبعه-اناس-ثم-تاب
  • Imechapishwa: 21/08/2022