Mzimiaji amepewa maji wakati wa swawm

Swali: Kuna mtu mfungaji alizimia na kipindi alipokuwa katika hali hiyo akaanza kutokwa na povu mdomoni ambapo mtu aliyekuwa pambizoni mwake akammwagia maji mdomoni mwake. Je, amefungua?

Jibu: Ni jambo linalotambulika kuwa ambaye amepoteza fahamu na akamwagiwa maji kooni mwake hahisi jambo hilo. Lakini, je, swawm yake imeharibika? Kwa mujibu wa maoni yaliyotangaa ya madhehebu ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ni kwamba hafungui kwa sababu amemeza pasi na kutaka kwake mwenyewe. Moja miongoni mwa sharti za vifunguzi vya swawm ni mfungaji aiharibu kwa kutaka kwake mwenyewe, jambo ambalo halikupatikana hapa. Baadhi ya wanazuoni wengine wamesema kuwa swawm inaharibika. Wengine wamesema kuwa swawm inaharibika ikiwa kimazowea ni mwenye kuridhia jambo hilo na akiwa si mwenye kuridhia basi swawm haiharibiki. Kinachodhiri ni yale maoni ya kwanza; swawm haiharibiki. Kujengea juu ya haya funga yake ni sahihi kwa sababu kwa sababu jambo hili limepitika pasi na kutaka kwake mwenyewe. Hata hivyo bora ni yeye kufunga siku nyingine badala ya siku hii. Kwa sababu kama inamlazimu kufanya hivo, basi itakuwa imetakasika dhimma yake, na kama haimlazimu, basi itazingatiwa kuwa ni swawm ya kujitolea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/276)
  • Imechapishwa: 06/05/2021