Mzee wa miaka 85 asiyeweza kufunga Ramadhaan

Swali: Mimi nina baba ambaye hajafunga kwa sasa miaka minne. Ni mwenye kulazwa juu ya kitanda. Ni mgonjwa. Umri wake unazidi miaka thamanini na tano. Je, analazimika kutoa kafara?

Jibu: Ndio. Mzee asiyeweza kufunga basi ni lazima kwake kutoa fidia kwa kila siku moja kulisha masikini. Atawalisha vipi? Ama awakusanye masikini hao katika chakula cha mchana, japo chakula cha mchana katika Ramadhaan huwa ni mgumu, au chakula cha jioni. Siku moja anawalisha masikini kumi, siku ya kufuatia masikini kumi wengine na siku ya tatu masikini kumi wa mwisho. Hii ni njia moja. Vilevile anaweza kumpa chakula kila mmoja 1,5 kg ikiambatana na nyama. Nyama hiyo inaweza kuwa ya ng´ombe, ya mbuzi/kondoo, ya ngamia au ya kuku.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1376
  • Imechapishwa: 30/11/2019