Mzee asiyeweza kufunga Ramadhaan


Swali: Kuna mama mzee sana ameshindwa kufunga Ramadhaan. Kumeshapita miaka mitatu yuko katika hali hii kutokana na utuuzima na maradhi. Ni lipi linalomlazimu?

Jibu: Mambo yakiwa hivo ulivyoeleza basi ni wajibu kwake kulisha kwa kila siku moja aliyoacha kufunga masikini. Anatakiwa kulisha nusu pishi katika mchele, tende, mahindi au vyengine ambavyo anawalisha familia yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/161)
  • Imechapishwa: 04/06/2017