Mzee anataka kuwakilisha mtu amhijie hajj ya sunnah

Swali: Kuna mtu anataka kuhiji hajj ya sunnah. Lakini hata hivyo hawezi kwa sababu ya ukubwa utuuzima wake. Bora ni yeye kuwakilisha mtu amhijie au atoe swadaqah kile kiwango?

Jibu: Bora ni yeye kuteua mtu ambaye atahiji faradhi kwa pesa hizi. Asiwakilishe mtu amhijie. Kwa sababu kuwakilisha mtu amuhijie mwingine ni jambo limepokelewa kuhusu hajj ya faradhi na sio hajj iliyopendekezwa. Asipopata mtu ambaye anahitajia kuhiji hajj ya faradhi, basi azitumie pesa hizi katika kujenga msikiti, tendo jema jingine au azimpe swadaqah fakiri au ndugu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1434
  • Imechapishwa: 27/12/2019