Mzee ameshindwa kufunga kwa sababu ya utuuzima na maradhi sugu


Swali: Mimi ni mzee niliye na miaka themanini ambaye niko na maradhi kwenye mshipa na maradhi ya moyo. Sikuweza kufunga Ramadhaan ya mwaka 1404 uliyopita. Nimetoa mifuko mitatu kwa familia tatu zinazohitajia zinazopatikana katika kijiji chetu. Jumla ya hiyo mifuko mitatu ni Mudd[1] thelathini na nne. Mwaka huu pia sijui kama naweza kufunga au siwezi. Kwa ajili hiyo naomba mnipe fatwa kwa yale niliyokuelezeni kwa kuwa mimi sina amani isipokuwa baada ya kupata fatwa yenu.

Jibu: Mambo yakiwa kama ulivyotaja ya kwamba una miaka themanini na kwamba una maradhi ya kwenye mshipa na ya moyo na kuwa Ramadhaan iliyopita uliacha kufunga kwa sababu ya kutoweza kufunga, hakuna neno kula. Inatosheleza kulisha masikini mmoja kwa kila siku moja uliyoacha kufunga. Kiwango chake ni nusu pishi ambayo kiasi chake ni takriban 1,5 kg katika mchele, ngano na vyakula vyengine ambavyo vimezoeleka katika nchi yenu.

[1] Imaam ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: ”Mudd ni sawa na kama robo hivo.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah (02/252) iliyochapishwa na Daar Ibn-ul-Jawziy).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/166-167)
  • Imechapishwa: 04/06/2017