Swali: Kuna mtu ana watoto watatu ambao hawana mapungufu katika kumtii na kumtendea wema, na yeye (mzazi huyo) anawaombea dhidi yao. Je, Du´aa yake itawadhuru?

Jibu: Haimpasi muumini kuomba dhidi ya watoto wake, bali ni wajibu kwake kutahadhari kwa hilo, kwa kuwa anaweza kuomba katika saa ya kujibiwa. Haimpasi kwake kuomba dhidi yao, na ikiwa ni wema jambo hili linakuwa baya zaidi kukosa kuwaombea Du´aa. Ama ikiwa wana mapungufu, haitakikani vilevile kwake kuomba dhidi yao. Bali kinyume chake, awaombee uongofu na wema na Tawfiyq. Namna hii ndivyo inavyopasa kuwa kwa muumini. Na kumekuja nususi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo zinatahadharisha mzazi kumuombea Du´aa mbaya mtoto wake, ahli zake na mali yake. Kwa kuwa anaweza kuomba saa ya kujibiwa, akawa amejidhuru nafsi yake mwenyewe, ahli zake na mtoto wake. Inatakikana kwako ewe muulizaji uuhifadhi ulimi wako na umkataze unayemjua kuwa anafanya jambo hili auhifadhi ulimi wake na amche Allaah kwa hilo, mpaka asiombe dhidi ya mtoto wake wala kuwaombea Waislamu wengine. Bali kinyume chake, awaombee kheri, uiamara na msimamo. Na isiwe kuwaombea Du´aa dhidi yao kwa yanayowadhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb (770)
  • Imechapishwa: 16/03/2018