Mzazi ameacha kulipa deni la Ramadhaan kwa miaka mingi kwa ujinga

Swali: Nilikuwa naishi katika kijiji ambacho hakijui hukumu ya kulipa deni la Ramadhaan. Nikaishi huko kwa muda mrefu na nikazaa watoto watatu. Halafu nikarudi Jeddah na nikajua kuwa kulipa deni la Ramadhaan ni wajibu. Ni lipi linalonilazimu hivi sasa kwa vile sijui ni idadi ya siku ngapi ambazo ni wajibu kwangu kulipa? Je, zinanigusa hukumu za kulipa pamoja na kwamba nilikuwa katika kijiji kisichokuwa cha Kiislamu kisichokuwa lolote kuhusiana na suala hili?

Jibu: Ikiwa mwanamke huyu alikuwa hajui kuwa swawm ya Ramadhaan ni faradhi na anakula siku moja na kufunga siku moja hakuna linalomlazimu wala kulipa. Kwa sababu maoni yenye nguvu ni kuwa Shari´ah haimlazimu mtu kabla ya kujua. Huyu alikuwa katika kijiji kisichokuwa cha Kiislamu na hajui lolote kuhusiana na Uislamu na hivyo haimlazimu kwake kulipa.

Ama ikiwa alikuwa anajua kuwa swawm ya Ramadhaan ni wajibu lakini hata hivyo akafanya uvivu wanachuoni wana maoni mawili kuhusiana na hali hii:

Ya kwanza: Kuna waliosema kuwa ni wajibu kwake kulipa.

Ya pili: Wengine wakasema kuwa sio wajibu kwake kulipa kwa sababu alifanyia kusudi kuchelewesha faradhi iliyowekwa kwa wakati wake na kila ambaye atafanyia kusudi kuchelewesha faradhi iliyowekwa kwa wakati wake haisihi kuilipa.

Lakini kinachonidhihirikia kutokana na hali ya muulizaji ni kwamba hakufanya yote mawili. Kujengea juu ya hili haimlazimu kulipa maadamu hakuwa anajua kuwa Ramadhaan wala kulipa ni wajibu. Katika hali haimlazimu kupa kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru kwa ujinga wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (25)
  • Imechapishwa: 14/01/2019