Mwombe Allaah akupe uombezi wa Mtume Wake  

Swali: Je, inajuzu kwa mtu kuomba kwa du´aa hii “Ee Allaah! Usininyime uombezi wa watu wema siku ya Qiyaamah” au akakhusisha kwa kusema “Ee Allaah! Usininyime uombezi wa mwanachuoni fulani siku ya Qiyaamah?”

Jibu: Aombe kutoka kwa Allaah ampe uombezi wa Mtume. Ikiwa anataka kuomba kutoka kwa kiumbe basi amuombe Allaah ampe uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2104
  • Imechapishwa: 28/06/2020