Swali: Wakati nilipokuwa kijana nilichukua pesa za watu kwa dhuluma. Nifanye nini kwa sababu siwajui watu hao?

Jibu: Ikiwa huwajui na wala huwezi kuwafikishia pesa zao, zitoe swadaqah kwa lengo thawabu ziwaendee wenye nazo. Kazi yako unatakiwa kujikwamua na pesa hizo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 04/03/2022